China yapiga hatua katika utafiti wa dawa za kutibu COVID-19
2021-09-14 15:21:41| cri

 

 

Shirika la Matibabu na Dawa la China (Sinopharm) limetangaza kuwa limepiga hatua katika utafiti wa dawa mbili za COVID-19, ambazo zinafaa kwa wagonjwa walio na hali nzuri.

Mwanasayansi mkuu wa Kampuni ya Teknolojia ya Viumbe ya China iliyo chini ya Sinopharm Bw. Zhang Yuntao, amesema dawa hizo zinazotengenezwa kulingana na kinga ya mwili na antibody monoclonal, zinatumiwa kupunguza kiwango cha virusi mwilini mwa wagonjwa.

Bw. Zhang amesema dawa hizo zimeonesha ufanisi wa kutibu wagonjwa wenye dalili za kiwango cha chini na katikati katika matumizi ya dharura.