Maelezo mafupi kuhusu riwaya ya Tata za Asumini
2021-09-14 13:51:04| cri

Kwenye Riwaya ya Tata za Asumini ambayo imeandikwa na Mwandishi Said A. Mohamed mhusika mkuu ni Asumini ambaye anajipata kwenye hali ngumu ya dunia chafu iliojaa utata, naye amenaswa kwenye tata hizo tokea mwanzo hadi mwishi. Maisha yake yamejaa vuta nikuvute. Amejipata kwenye njia-panda. Nafsi yake kwa undani inamtaka afuate maadili ya malezi mema na nje nafsi nyingine inamvuta kuingia kwenye dunia chafu –mwishoye anararukararuka.