Maendeleo ya wanawake katika sekta ya sayansi
2021-09-16 14:41:15| CRI

Maendeleo ya wanawake katika sekta ya sayansi_fororder_VCG111301846219

Tarehe Mosi Oktoba ya kila mwaka ni Siku ya Taifa la China. Nchi hiyo ambayo imekuwa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, imesherehekea miaka 72 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Katika kipindi hicho, chini ya uongozi wa thabiti wa Chama cha kikomunisti cha China, nchi hiyo imepata maendeleo makubwa yanayoshangaza jamii ya kimataifa. Maendeleo hayo ni katika sekta mbalimbali za biashara, uchumi, afya, miundombinu, uchukuzi, na katika sayansi na teknolojia. katika kipindi cha leo, tutaangalia zaidi maendeleo ya wanawake katika sekta ya sayansi, sio hapa China tu, bali hata katika nchi nyingine hususan za Afrika.