Rais Xi Jinping atangaza kufunguliwa rasmi kwa Michezo ya 14 ya Taifa
2021-09-16 08:54:14| cri

Rais Xi Jinping atangaza kufunguliwa rasmi kwa Michezo ya 14 ya Taifa_fororder_VCG111348351341

Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano alitangaza kufunguliwa rasmi kwa Michezo ya 14 ya Taifa, inayofanyika mjini Xi’an mkoani Shaanxi.

Sherehe kubwa ya ufunguzi iliyojumuisha muziki, ngoma na maonesho ya kiutamaduni ilifanyika kwenye Uwanja wa Kituo cha Olimpiki cha Xi’an. Chini ya kauli mbiu ya “Michezo kwa wote, pamoja kwa akili na vitendo”, mashindano hayo yanashirikisha jumla ya michezo 54 yakiwemo matukio 595, ambapo michezo 35 na matukio 410 yamepangwa kwa ajili ya wanariadha bingwa na mingine iliyobaki ni michezo inayojumuisha watu wote. Michezo hiyo inayoshirikisha wanariadha zaidi ya 12,000 itakamilika Septemba 27.