Maafisa wa masuala ya kibinadamu wana wasiwasi juu ya hali ya kaskazini mwa Ethiopia
2021-09-16 09:32:59| cri

Wafadhili wa Umoja wa Mataifa wanaoshughulikia masuala ya kibinadamu jana walionyesha wasiwasi wao juu ya hali ya eneo la kaskazini mwa Ethiopia.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuwa hali ya kibinadamu katika mkoa wa kaskazini mwa Tigray bado ni mbaya, na hali katika maeneo jirani ya Amhara na Afar pia inazidi kuwa mbaya. Kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 7 mwezi Septemba, malori 147 ya misaada ya kibinadamu yalifika Tigray kupitia Afar. Kabla ya hapo, hakuna malori yaliyoweza kuingia Tigray tangu tarehe 22 mwezi Agosti.

Ameongeza kuwa hatua hii ni nzuri, lakini malori 100 ya chakula, vitu visivyo vya chakula na mafuta lazima yaingie Tigray kila siku ili kukidhi kiwango cha mahitaji kwenye maeneo hayo. Vifaa vingine havijaweza kuingia kabisa, pamoja na mafuta, ambapo bila ya vifaa hivyo shughuli zao zinakuwa vigumu kuendelea.