Mwakilishi wa China katika UM alaani baadhi ya nchi za magharibi kukiuka haki za binadamu
2021-09-17 10:25:05| cri

Balozi wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Jiang Duan ameeleza kuwa, nchi nyingi za magharibi zilikiuka vibaya haki za binadamu katika historia ya kisasa. Ingawa ukweli unajulikana, lakini nchi hizo hazijawajibika.

Balozi Jiang alisema hayo wakati akihutubia Mkutano kuhusu suala la haki za ukweli wa mambo katika Kikao cha 48 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Katika hotuba hiyo balozi Jiang amesema baadhi ya nchi za magharibi ziliwaua wenyeji wa asili huku zikiingilia kati kijeshi katika nchi nyingine, hatua ambazo zimekiuka vibaya haki za binadamu, na kwamba China inatoa wito kwa jamii ya kimataifa na nchi husika kuyatizama kwa jicho sahihi masuala hayo, na kuwajibisha watu waliofanya uhalifu kwa vitendo halisi.