China, Russia, Pakistan na Iran kuimarisha uratibu kuhusu suala la Afghanistan
2021-09-17 10:26:07| cri

Mawaziri wa mambo ya nje wa China, Russia na Pakistan na msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Iran wamekubaliana kuongeza mawasiliano na uratibu juu ya suala la Afghanistan kwenye mkutano wao usio rasmi kuhusu Afghanistan uliofanyika Dushanbe, mji mkuu wa Tajik.

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema ni muhimu kwa nchi hizi nne kuongeza mawasiliano na uratibu, kutoa kauli moja, kutoa ushawishi chanya, na kuonesha nafasi ya kiujenzi katika kutuliza hali ya Afghanistan.

Amesisitiza kuwa nchi za kanda hii zinatarajia kuwa serikali mpya ya Afghanistan itakuwa jumuishi, kupambana na ugaidi na kuwa mwema kwa nchi jirani.