Serikali ya mkoa wa Xinjiang yasema njama za kuhujumu utulivu wa mkoa huo kamwe hazitafanikiwa
2021-09-17 15:46:16| cri

Serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauigur wa Xinjiang leo hapa Beijing imefanya mkutano na wanahabari kuhusu suala la mkoa huo, ambapo imesisitiza kuwa njama yoyote ya kuhujumu utulivu na maendeleo ya Xinjiang kamwe haitafanikiwa.

Kwenye mkutano huo, msemaji wa serikali ya Xinjiang Bw. Eljan Anayt amesema, suala la Xinjiang sio suala la kabila, dini au haki za binadamu, bali ni suala la kupambana na ufarakanishaji, ugaidi na itikadi kali. Ameongeza kuwa, hatua zilizochukuliwa na China kuondoa itikadi kali zimefanikiwa kuzuia kutokea kwa matukio ya kigaidi na kimabavu mkoani humo, na hivyo kuhakikisha wakazi wa makabila mbalimbali wa mkoa wa Xinjiang wanaishi kwa amani na usalama. Mafanikio hayo yametambuliwa na kupongezwa na jumuiya ya kimataifa.

Msemaji huyo amesema, njama za baadhi ya wanasiasa na makundi ya nchi za nje ya kuipinga China za kutaka kuhujumu utulivu na maendeleo ya Xinjiang kwa kupitia kuuchafua mkoa huo na kusambaza taarifa potofu kuhusu hali ya mkoa huo kwa kisingizio cha haki za binadamu, kamwe hazitafanikiwa.