Rais wa China asema hatma ya Afghanistan inatakiwa kuwa mikononi mwa watu wake
2021-09-17 19:47:24| cri

Rais Xi Jinping wa China ameshiriki kwa njia ya video kwenye mkutano wa pamoja wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano la Shanghai (SCO) na nchi wanachama wa Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO) kuhusu suala la Afghanistan. Rais Xi amesema, zikiwa nchi jirani wa Afghanistan, wanachama wa SCO na CSTO, nchi hizo zinnapaswa kuchukua jukumu pamoja kudumisha amani na utulivu wa Afghanstan. Rais Xi amesisitiza kuwa mustakabali wa Afghanistan unapaswa kuwa mikononi mwa watu wote wa Afghanistan.