Wanaanga waliokwenda anga za juu na Chombo cha Shenzhou No.12 warudi salama duniani
2021-09-17 15:06:28| cri

Wanaanga waliokwenda anga za juu na Chombo cha Shenzhou No.12 warudi salama duniani_fororder_1127873155_16318618335681n

Chombo cha Shenzhou No. 12 cha China kilichobeba wanaanga watatu kimetua salama katika eneo la kutua la Dongfeng katika mkoa wa Mongolia ya Ndani. Wanaanga hao Bw. Yang Hongbo, Bw. Nie Haisheng na Bw. Liu Boming wametoka katika chombo hicho na wana hali nzuri ya kiafya.

Wanaanga hao wamekaa kwenye kituo cha anga za juu cha China kwa miezi mitatu, muda ambao ni mrefu zaidi kwa safari moja katika historia ya safari za anga za juu ya China.