Tamasha la Sikukuu ya Mwezi la CMG kuonyeshwa nje ya China kwa mara ya kwanza
2021-09-19 20:20:15| Cri

Tamasha la Sikukuu ya Mwezi la Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) litaonyeshwa tarehe 21 mwezi huu, ambalo litaonyeshwa kwa mara ya kwanza nje ya China kwa wakati mmoja .

Ili kuwafahamisha kwa kina watazamaji wa nchi za nje utamaduni wa China, tamasha hilo la CMG litaonyshwa kwa wakati mmoja kwenye televisheni za nchi za nje kwa mara ya kwanza, ikiwa ni pamoja na Switch TV ya Kenya. Tamasha hilo litaelezwa kwa lugha ya Kiingereza, ili kuwafahamisha watazamaji desturi ya Sikukuu ya Mwezi, historia ya tamasha hilo, na mada ya tamasha la mwaka huu.