Watu watano wajeruhiwa katika ajali ya kuanguka kwa ndege ya mafunzo ya kijeshi huko Texas, Marekani
2021-09-20 09:34:57| CRI

Watu watano wamejeruhiwa katika ajali ya kuanguka kwa ndege ya mafunzo ya kijeshi iliyotokea kwenye eneo la makazi katika Ziwa Worth, jimbo la kusini la Texas nchini Marekani.

Habari kutoka kwa kituo cha habari cha Fort Worth Star-Telegram, zinasema watu wawili walitoka nje kutoka ndege hiyo na kupelekwa katika hospitali za eneo hilo, mmoja akiwa mahututi na mwingine akiwa amejeruhiwa vibaya.

Watu wengine watatu waliojeruhiwa ardhini walitibiwa na kuondoka hospitali.