China kuiunga mkono kithabiti Russia kupata mafanikio mapya chini ya uongozi wa rais Putin
2021-09-20 21:24:10| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema ikiwa mwenzi wa uratibu wa kimkakati wa Russia katika pande zote, China itaendelea kuunga mkono kithabiti watu wa Russia kuamua wenywe njia ya maendeleo, na pia Russia kupata mafanikio mapya chini ya uongozi wa rais Vladimir Putin.

Russia ilifanya uchaguzi wa bunge la Duma kuanzia tarehe 17 hadi 19, Septemba. Kwa mujibu wa matokeo ya awali, Chama cha United Russia kinatarajiwa kushinda uchaguzi huo. Juu ya hilo, Bw. Zhao amesema uchaguzi wa bunge la Duma ni shughuli kubwa ya kisiasa ya taifa la Russia, na matokeo ya uchaguzi yameonesha maoni ya watu wa Russia. Ameongeza kuwa baada ya bunge jipya kuchaguliwa, China inapenda kuimarisha ushirikiano kati ya mabunge ya nchi hizi mbili, kuhimiza mawasiliano kati ya vyama vya pande mbili na kukuza zaidi uhusiano kati ya China na Russia katika zama mpya.