CMG kuwa vyombo vya habari pekee mshirika vya kichina vya Maonyesho ya Expo 2020 Dubai
2021-09-20 21:26:14| cri

Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG limesaini mkataba na kampuni ya Maonyesho ya Expo 2020 Dubai na kuwa vyombo vya habari pekee mshirika vya kichina vya Maonyesho hayo. Pande hizi mbili zimekubaliana juu ya eneo maalum la kufanyia kazi, nembo ya Maonyesho hayo na jinsi ya kutumia maudhui ya maonyesho pamoja na haki miliki za ubunifu.