Tanzania yashuhudia ongezeko la miradi mipya ya uwekezaji wakati maambukizi ya COVID-19 yakiendelea nchini humo
2021-09-20 09:42:11| CRI

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa amesema idadi ya miradi mipya ya uwekezaji iliyoandikishwa nchini Tanzania kati ya Machi na Agosti mwaka huu imeongezeka hadi 133, na thamani yake ni dola bilioni 2.98 za kimarekani.

Bw. Msigwa amesema miradi mipya ya uwekezaji iliyoandikishwa na kituo cha uwekezaji cha Tanzania TIC inatarajiwa kutoa nafasi za ajira kwa watu 29,709.

Ofisa huyo amesema ongezeko hilo linatokana na mageuzi makubwa yanayofanywa na rais Samia Suluhu Hassan yakiwa na lengo la kurahisisha mazingira ya uwekezaji.