Serikali kuu ya China yapongeza tume ya uchaguzi ya serikali ya utawala maalum ya Hong Kong kwa uchaguzi wenye mafanikio
2021-09-20 09:07:54| CRI

Serikali kuu ya China yapongeza tume ya uchaguzi ya serikali ya utawala maalum ya Hong Kong kwa uchaguzi wenye mafanikio_fororder_VCG111348979526

Msemaji wa serikali kuu ya China amepongeza kufanyika kwa mafanikio uchaguzi wa wajumbe wa tume ya uchaguzi mkoani Hong Kong na kutaja mafanikio hayo kuwa ni mwanzo wa matarajio mapya na yanaleta matumaini mapya.

Msemaji wa ofisi ya serikali inayoshughulikia mambo ya Hong Kong na Macau amesema uchaguzi huu ni uchaguzi wa kwanza muhimu kufanyika, tangu ipitishwe sheria ya kulinda usalama wa taifa ya Hong Kong mwaka 2020.

Amesema uchaguzi huo ni mfano wazi wa kutekeleza kanuni ya “watu wa Hong Kong kuiongoza Hong Kong” na inaleta matarajio mapya kwa Hong Kong kuendelea na utulivu na maendeleo.

Msemaji huyo amesema, baada ya idadi ya wajumbe wa tume ya uchaguzi kuongezeka kutoka 1,200 hadi 1,500 na njia ya uundwaji wake kuboreshwa, tume hiyo sasa imekuwa na uwakilishi mkubwa zaidi.