Mbalamwezi na ndoto
2021-09-21 10:41:16| cri

Mbalamwezi na ndoto_fororder_微信图片_20210921104235

Leo ni sikukuu ya mwezi nchini China. Kwa mujibu wa desturi ya Kichina, siku hiyo ni siku ya kutimiza ndoto. Katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uongozi imara wa rais Xi Jinping, China imetimiza ndoto moja baada ya nyingine.

Ndoto ndio mwanzo wa juhudi zote.

Mwezi Novemba mwaka 2012, kwenye Uwanja wa Tiananmen mjini Beijing, rais Xi alitangaza kuwa China itatimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora ifikapo mwaka wa 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Mbalamwezi na ndoto

Mwezi Julai mwaka 2021, pia kwenye huohuo wa Uwanja wa Tiananmen, wakati wa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC, rais Xi alitangaza kwamba lengo hilo ambalo ni lengo la kwanza la miaka 100 la China, limetimizwa.

Mbalamwezi na ndoto

Ndoto ni nguvu ya kusonga mbele.

Mwaka 2021, China ilifanikiwa kujenga “nyumba” kwenye anga ya juu, ambayo ni ndoto ya muda mrefu ya taifa la China.

Mbalamwezi na ndoto

Tarehe 23 Juni mwaka huu, rais Xi alitembelea Kituo cha Usimamizi wa Usafiri wa Anga ya Juu cha Beijing na kuzungumza na wanaanga Nie Haisheng, Liu Boming, na Tang Hongbo ambao walikuwa kwenye kituo cha anga za juu cha China, na kusema wao ni wawakilishi hodari wa China wanaoshughulikia masuala ya anga ya juu katika enzi mpya.

Mbalamwezi na ndoto

Ndoto ni shahidi wa maendeleo ya taifa la China.

Ndoto ya Olimpiki ya China iliyoendelea kwa karne moja imeshuhudia juhudi na maendeleo ya taifa la China. Mwaka 2008, China ilitimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto iliyofanyika mjini Beijing.

Mbalamwezi na ndoto

Mwaka 2022, mji wa Beijing utaandaa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, na kuufanya mji huo kuwa wa kwanza duniani kuandaa michezo hiyo miwili ya Olimpiki.

Mbalamwezi na ndoto

Kutoka Sochi hadi Lausanne, kutoka Chongli hadi Beijing, rais Xi amefuatilia sana Michezo ya Olimpiki. Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach alisema, anatumaini kumpa Rais Xi medali ya dhahabu kwa mchango wake wa kuhimiza maendeleo ya Olimpiki.

Mbalamwezi na ndoto

Ndoto za Wachina zinatimizwa katika ardhi ya zaidi ya kilomita milioni 9.6 za mraba nchini China. Sasa Chama cha Kikomunisti cha China kinawaongoza wananchi wake kufanya juhudi za kutimiza lengo la pili la miaka 100, ambalo ni kwamba, itakapofika mwaka wa 100 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, nchi hiyo itakuwa nchi ya kijamaa yenye nguvu, demokrasia na ustaarabu mkubwa.

Kama njia ni sahihi, umbali sio tatizo.