Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China yafikia nchini Denmark kwa ajili ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa
2021-09-21 09:23:30| cri

Shehena ya chanjo ya COVID-19 ya Sinopharm iliyotolewa na serikali ya China kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa imefika huko Copenhagen, Denmark Jumatatu wiki hii.

Naibu mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa la China Zhang Maoyu, amesema kwenye hafla ya kukabidhi chanjo hiyo iliyofanyika Ijumaa kwa njia ya mtandao kuwa chanjo hiyo zinatarajiwa kutolewa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walio mstari wa mbele na washirika wa karibu kwenye maeneo ya operesheni barani Afrika.

Katibu mkuu msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayesimamia usambazaji wa vifaa Christian Francis Saunders, amesema msaada huo wa China utaongeza uwezo wa Umoja wa Mataifa kukabiliana na janga la virusi vya Corona na kusaidia walinda amani kutekeleza majukumu yao vizuri zaidi.