Rais Xi ahutubia mjadala wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu la UM
2021-09-22 09:40:39| CRI

Rais Xi ahutubia mjadala wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu la UM_fororder_1127886752_16322544640581n (1)

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mjadala wa kawaida wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao, na kutoa hotuba muhimu kuhusu “kuimarisha nia, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, na kujenga dunia nzuri zaidi kwa pamoja”.

Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema huu ni mwaka wa 50 tangu Jamhuri ya Watu wa China irejee kwenye Umoja wa Mataifa, na China itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na umoja huo, na kutoa mchango zaidi kwa shughuli zake.

Rais Xi amehimiza jumuiya ya kimataifa kushinda janga la COVID-19, kufufua uchumi, kuimarisha mshikamano, kuboresha usimamizi wa mambo ya kimataifa na kutekeleza utaratibu halisi wa pande nyingi.

Amesema China siku zote imekuwa ikirithisha na kufuata dhana ya amani na masikilizano, haikuvamia na haitavamia nchi nyingine, na kufanya umwamba. Ameongeza kuwa mafanikio ya nchi moja hayamaanishi kushindwa kwa nchi nyingine, na dunia inaruhusu maendeleo ya pamoja ya nchi zote.

Aidha rais Xi amesisitiza kuwa demokrasia sio hataza ya nchi fulani, bali ni haki ya watu wa nchi zote, na dunia inapaswa kuwa na staarabu anuwai.