China yapinga Marekani kuweka vikwazo vipya dhidi ya Ethiopia
2021-09-23 09:10:02| CRI

Hivi karibuni Rais Joe Biden wa Marekani alitangaza kuiwekea  vikwazo vipya Ethiopia kutokana na mgogoro nchini humo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema kwenye mkutano wa kawaida na waandishi wa habari kwamba China inapinga Marekani kuweka vikwazo hivyo dhidi ya Ethiopia.

Bw.Zhao Lijian amesema kuwa China siku zote inasisitiza nchi mbalimbali kufuata sheria za kimataifa na kanuni za msingi za mahusiano ya kimataifa, na kupinga vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine kupitia kuiwekea vikwazo au kutishia kuiwekea vikwazo. Amesema Marekani inapaswa kushughulikia kwa makini maswala yanayohusiana na Ethiopia, na kufanya kazi za kijenzi kwa ajili ya kurudisha amani na utulivu nchini Ethiopia.