Baraza kuu la UM laridhia azimio la kisiasa kuhusu mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi
2021-09-23 08:30:34| CRI

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumatano liliridhia azimio la kisiasa kuhusu mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kuadhimisha miaka 20 tangu kupitishwa kwa Azimio la Durban na Mpango wake wa Utekelezaji.

Azimio hilo la kisiasa linathibitisha tena kuwa Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji na nyaraka zilizofuata vinaweka mfumo wa jumla wa Umoja wa Mataifa, na msingi imara wa kupambana na ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na matatizo husika, na kusisitiza ahadi ya nchi wanachama kutekeleza azimio hilo kikamilifu na kwa ufanisi.

Azimio hilo limetoa wito kwa nchi zote, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda na kimataifa na kuwaalika wadau wote wanaohusika kubeba wajibu wao na kuongeza juhudi kwa ajili ya kutokomeza aina zote za uchaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na matatizo yanayohusika, na kuendeleza ushirikiano na mashirika yote husika ya Umoja wa Mataifa ya kulinda haki za binadamu.