Busara katika macho yake
2021-09-27 11:03:45| cri

Mwezi Machi mwaka 2013, kabla ya kufanyika kwa mkutano wa tano wa viongozi wa nchi za BRICS, rais Xi Jinping wa China alihojiwa na wanahabari wa kigeni. Mmoja kati ya waandishi hao alikuwa ni naibu mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Shirika la habari la ITAR-TASS Mikhail Gusman. Mambo mawili yalimvutia mwanahabari huyo mkongwe wa Russia, ambayo ni busara aliyoiona machoni mwa kiongozi huyo wa China, na nguvu ya kupeana mikono yake. Kama mtu aliyefuatilia kwa karibu kazi ya rais Xi, Gusman amevutiwa zaidi na jinsi alivyoshughulikia mgogoro wa COVID-19.