Rais Xi Jinping atoa hotuba kwenye ufunguzi wa baraza la Zhongguancun
2021-09-24 20:47:52| cri

Rais Xi Jinping wa China leo amehutubia sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa baraza la Zhongguancun 2021 kwa njia ya video.

Mkutano wa mwaka huu wenye kaulimbiu ya "akili, afya na bila kaboni," unaanza leo Ijumaa na utafanyika hadi Jumanne.

Baraza la Zhongguancun lilianzishwa mwaka 2007 na limekua jukwaa la kitaifa la uvumbuzi wa wazi na baraza la kimataifa la uvumbuzi.