China yatoa waraka kuhusu maendeleo ya idadi ya watu ya Xinjiang
2021-09-26 13:57:24| cri

China yatoa waraka kuhusu maendeleo ya idadi ya watu ya Xinjiang_fororder_IMG_5002(20210926-134210).JPG

Ofisi ya Habari ya Baraza la serikali ya China leo imetoa waraka unaoelezea maendeleo ya idadi ya watu katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur.

Ongezeko la idadi ya watu wa Xinjiang ni la juu kuliko wastani wa taifa

Ongezeko la idadi ya watu katika mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa China wa Xinjiang Uygur kuanzia mwaka 2000 hadi 2020, lilikuwa asilimia 1.15 juu kuliko wastani wa taifa katika kiwango cha ongezeko la jumla kwa mwaka.

Idadi ya watu wa kabila la Uygur iko katika kiwango cha juu cha ukuaji

Idadi ya watu wa kabila la Uygur iliongezeka kwa kiwango cha asilimia 1.67 kwa mwaka kwa muda wa miongo miwili ya kwanza ya karne ya 21 kutoka watu zaidi ya milioni 8.34 hadi zaidi ya milioni 11.62.

'Kutumikishwa kwa kulazimishwa' ni uongo unaotumiwa na watu wanaoipinga China ili kuchochea shida huko Xinjiang

Kupitia uwongo huo, makundi ya watu wanaoipinga China wanapaka matope hatua zinazochukuliwa na China kwenye kupambana na ugaidi na msimamo mkali, kukwamisha uendelezaji wa sekta mbalimbali za Xinjiang kama pamba, uzalishaji wa nyanya, na bidhaa za nitati ya jua, na kudhoofisha ushiriki wa China katika ushirikiano kwenye mnyororo wa viwanda duniani.

Hadhi ya kijamii ya wanawake wa Xinjiang inaendelea kuboreka

Hadhi iliyoboreshwa ya wanawake, imewawezesha kupata fursa zaidi ya elimu ya sekondari na ya juu, na kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii.

Madai ya “Mauaji ya halaiki” huko Xinjiang hayana msingi wowote

Xinjiang inatekeleza sera ya uzazi wa mpango kwa mujibu wa sheria, na kulazimishwa kudhibiti uzazi na vipimo vya ujauzito ni marufuku. Ni uamuzi binafsi wa watu kutumia dawa za uzazi wa mpango na jinsi ya kuzitumia. Hakuna shirika au mtu anayeweza kuingilia uhuru huo.

Shule za bweni huko Xinjiang zinajumuisha upatikanaji wa elimu kwa wote

Kuanzisha shule za bweni ni jambo la kawaida katika elimu ya lazima ya China, na ni juu ya familia za wanafunzi kuamua kama wanapenda au la.

Lugha, tamaduni za makabila madogo huko Xinjiang vinalindwa vizuri

Wakati wa kutekeleza ufundishaji wa lugha ya kichina sanifu, Xinjiang pia pia inatoa mafunzo ya lugha ya za Uygur, Khazak, Kirgiz, Mongolia, Xibe na lugha nyingine katika shule za msingi na sekondari.

Xinjiang inaheshimu na inalinda uhuru wa imani ya dini

Waumini wako huru kushiriki katika shughuli halali za kidini, pamoja na kuabudu, kufunga, na kuadhimisha sherehe za kidini kulingana na mafundisho ya dini, kanuni na mila, katika nymba za ibada au majumbani mwao.

Tuhuma za "mauaji ya halaiki" ya Xinjiang zinafichua mawazo ya kimwamba ya makundi yanayoipinga China

Tuhuma za "mauaji ya halaiki" huko Xinjiang hazina ukweli wowote. Hawajui lolote kuhusu sera ya Xinjiang ya China, na mafanikio yaliyopatikana katika kuendeleza eneo hilo, na vitendo vyao ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa.