Rais Xi Jinping atoa pongezi kwa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Internet Duniani 2021
2021-09-26 14:41:23| cri

Rais Xi Jinping atoa pongezi kwa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Internet Duniani 2021_fororder_VCG111350714950

Rais Xi Jinping wa China leo Jumapili ametoa pongezi kwa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Internet Duniani wa mwaka 2021.

Rais Xi ameainisha kuwa teknolojia ya dijitali imeingia kikamilifu kwenye sekta zote na mchakato wote wa binadamu kuendeleza uchumi, siasa, utamaduni, jamii na ustaarabu wa ikolojia, na kutoa athari pana na za kina kwa maisha na uzalishaji mali wa binadamu. Kutokana na mabadiliko makubwa na janga kubwa vinavyoshuhudiwa duniani, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuungana mikono na kufuata mwelekeo wa maendeleo ya dijitali, mtandao na akili bandia, kushikilia vizuri fursa na kukabiliana na changamoto kwa pamoja.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikana na nchi mbalimbali duniani, kubeba kwa pamoja jukumu la kihistoria la kusukuma mbele maendeleo ya binadamu, kutia uhai uchumi wa kidijitali, kuimarisha ufanisi wa Serikali Mtandao, kuboresha mazingira ya jamii ya kidijitali, kuanzisha ushirikiano wa kimataifa kwenye sekta ya dijitali, na kuimarisha ulinzi na usalama wa kidijitali, ili kuufanya ustaarabu wa kidjitali unufaishe watu wa kila nchi, na kusukuma mbele ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.