Semina ya nne ya nadharia za vyama vya siasa vya China na Afrika yafanyika Beijing
2021-09-26 13:58:43| CRI

Semina ya nne ya nadharia za vyama vya siasa vya China na Afrika yafanyika Beijing_fororder_24032368

Semina ya nne ya nadharia za vyama vya siasa vya China na Afrika yafanyika Beijing_fororder_911041096

Semina ya nne ya nadharia za vyama vya siasa vya China na Afrika yafanyika Beijing_fororder_468461283

Semina ya nne kuhusu nadharia za vyama vya siasa vya China na nchi za Afrika imefanyika Septemba 24 mjini Beijing. Semina hiyo yenye kaulimbiu “Njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi: uvumbuzi na utendaji wa vyama vya siasa vya China na Afrika”, ilihudhuriwa na viongozi na wajumbe 300 wa vyama vya siasa kutoka nchi 14 za Afrika. Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Song Tao alihudhuria na kuhutubia ufunguzi wa semina hiyo iliyofanyika kwa njia ya video.

Kwenye hotuba yake, Bw. Song Tao alisema, suala la njia ya maendeleo ni suala muhimu la kinadharia na kiutendaji linaloamua kama nchi moja, taifa moja na chama kimoja kinaweza kupata mafanikio na ustawi au la, na mafanikio makubwa ya njia ya ujamaa wenye umaalum wa China yanatokana na uongozi imara wa CPC, ambacho kinaungwa mkono kithabiti na watu wa China.

Bw. Song Tao amesema, CPC siku zote kinashikilia kuunganisha maslahi ya watu wa China pamoja na maslahi ya binadamu wote, na njia ya China ya kujijenga kuwa nchi ya kisasa inayoongozwa na CPC imepanua njia ya nchi zinazoendelea kuelekea kuwa nchi za kisasa. Amesema vyama vya siasa vya China na Afrika, vikiwa ni waongoza njia na watungaji na watekelezaji wa sera za ndani na nje katika nchi zao, vinabeba jukumu muhimu la kutafuta na kuongoza njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi zao. Pande hizo mbili zinapaswa kuungana mkono katika njia zao za maendeleo kwa msingi wa kuheshimiana, kufundishana na kukubali tofauti zao, zikiendelea kuongeza uwezo wao wa kutumikia maslahi ya umma, na kusukuma mbele ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

Viongozi wa vyama vya kisiasa vya nchi za Afrika walioshiriki kwenye semina hiyo wakiwemo katibu mkuu wa Chama tawala cha Uganda (NRM) Bw. Richard Awany Todwong, naibu spika wa bunge la Afrika Kusini Bw. Lechesa Tsenoli, na kaimu katibu mkuu wa Chama tawala cha Sudan Kusini (SPLM) Bw. Peter Lam Both, wamepongeza maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC, na maadhimisho yajayo ya miaka 72 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Viongozi hao wanaona kuwa, mafanikio makubwa yaliyopatikana China chini ya uongozi wa CPC katika kukuza uchumi, kutokomeza umaskini na kupambana na janga la Corona, ni mfano wa kuigwa na nchi za Afrika, pia yanatoa motisha kwa vyama vya siasa vya Afrika kufuata kithabiti njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi zao. Pia wameeleza matarajio ya kuimarisha ushirikiano na CPC, ili kusukuma mbele zaidi mahusiano kati ya Afrika na China.