Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa kauli kuhusu kurudi nyumbani kwa Bibi Meng Wanzhou
2021-09-26 12:16:55| cri

Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa kauli kuhusu kurudi nyumbani kwa Bibi Meng Wenzhou_fororder_IMG_4999(20210926-115720).JPG

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China jana Bibi Hua Chunying ametoa maoni kuhusu kurudi nyumbani kwa Bibi Meng Wanzhou kutoka Canada. Amesema baada ya juhudi za serikali ya China, Bibi Meng aliondoka Canada Septemba 24, na hivi karibuni ataungana na familia yake. Akijibu swali wanahabari, msemaji huyo amesema msimamo wa upande wa China juu ya kesi ya Bibi Meng ulikuwa wazi na thabiti.

Amesema ukweli umethibitisha kuwa ilikuwa ni kesi ya kisiasa yenye lengo la kukandamiza kampuni za teknolojia ya hali ya juu za China. Amesema mashtaka dhidi ya Bibi Meng yaliyoitwa kuwa ni udanganyifu, si chochote isipokuwa uwongo tu. Amesema hata benki ya HSBC - "mwathiriwa" aliyetajwa na upande wa Marekani - imetoa mafaili yanayothibitisha kutokuwa na hatia kwa Bibi Meng. Amesema kilichofanywa na Marekani na Canada ni kesi ya kumuweka kizuini kiholela.