Tamasha la 17 la kimataifa la Katuni la China kufunguliwa Septemba 29
2021-09-27 14:25:22| Cri

Tamasha la 17 la kimataifa la Katuni la China kufunguliwa Septemba 29_fororder_0927 1

Tamasha la 17 la Kimataifa la Katuni la China litafanyika kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 4, 2021 mjini Hangzhou, mkoa wa Zhejiang, kusini mashariki mwa China.

Katika tamasha hili linaloandaliwa kwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), Idara Kuu ya Radio na Televisheni ya China na Serikali ya mkoa wa Zhejiang, kutakuwa na maonesho, mashindano ya chapa, mabaraza ya wataalamu pamoja na shughuli za biashara.

Tokea mwaka 2005, tamasha hilo limeshirikisha makampuni na mashirika zaidi ya elfu 17 na watu zaidi ya milioni 18 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 80 duniani.