Matangazo ya moja kwa moja ya CMG kuhusu kurudi kwa Meng Wanzhou nchini China yafuatiliwa sana duniani
2021-09-27 16:01:02| cri

Kutokana na juhudi za mfululizo za serikali ya China, Bi. Meng Wanzhou aliondoka Canada kwa ndege iliyokodiwa na serikali ya China mnamo tarehe 24 mwezi Septemba, akawasili mjini Shenzhen jioni ya tarehe 25, saa ya Beijing, na kurudi taifa la mama.

Saa nne dakika 29 sekonde 05 jioni ya tarehe 25 kwa saa za Beijing, APP ya habari ya CMG imetoa habari kwanza "Video ya kipekee: Bi. Meng Wanzhou yuko karibu kufika taifa la mama". Baadaye, APP ya habari ya CMG ilifanya kazi pamoja na kituo kikuu cha habari, kituo kikuu cha Amerika Kaskazini, na kituo kikuu cha Guangdong vimerekodi safari ya Bi. Meng kurudi kwa kupitia habari haraka 17 ya kipekee ambayo yalitokea kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wote.

Saa nne kabla ya kuwasili kwa ndege huko Shenzhen, shirika la CMG limefungua matangazo maalum ya moja kwa moja: Bi. Meng Wanzhou, karibu nyumbani! Matangazo yote ya moja kwa moja yanadumu kwa masaa 5. Hadi saa 6 usiku tarehe 25, jumla ya mara ya kutazamwa kwa matangazo hayo zilikuwa karibu milioni 430.

Mkurugenzi na mhariri mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema kuwa ripoti ya moja kwa moja ya CMG kuhusu kurudi kwa Bi. Meng Wanzhou ilisababisha majibu ya shauku kutoka kwa wanamtandao nchini kote. Chini ya matawi ya CMG kama CCTV, Client News Client, na CCTV.com, idadi ya kutoa Like kwa wanamtandao ilifikia milioni 400, ikizidi idadi ya watu wote wa Marekani na Canada.