Balozi wa Rwanda asema China imetimiza ahadi yake ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana na Afrika
2021-09-27 08:46:04| CRI

Balozi wa Rwanda asema China imetimiza ahadi yake ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana na Afrika_fororder___172.100.100.3_temp_9500031_1_9500031_1_1_8082d931-3275-401a-b952-69f16afeed1c

Maonesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yamefunguliwa mjini Changsha, China, na Rwanda ni moja ya nchi wageni rasmi wa maonesho hayo.

Balozi wa nchi hiyo nchini China James Kimonyo amesema, ushirikiano wa kunufaishana kati ya Afrika na China si wa maneno matupu, na China imetimiza ahadi yake kwa hatua halisi.

Balozi Kimonyo amesema, huu ni mwaka wa 50 tangu China na Rwanda zianzishe uhusiano wa kibalozi, na katika kipindi hicho, nchi hizo zimedumisha uhusiano wa kirafiki, na ushirikiano wao pia unasukumwa mbele katika nyanja mbalimbali. Ametolea mfano ujenzi wa miundombinu unaotekelezwa na China nchini Rwanda, na pia China kutoa ufadhili kwa wanafunzi wengi wa Rwanda kusomea nchini humo.

Ameongeza kuwa, wakati mlipuko wa janga la virusi vya Corona ulipotokea nchini Rwanda, China ilikuwa nchi ya kwanza kutoa msaada katika kukabiliana na janga hilo.

Aidha, Kimonyo amesema anatarajia kuwa uhusiano kati ya Rwanda na China utaendelea kupanuliwa katika siku zijazo.