Maonesho ya pili ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yafunguliwa
2021-09-27 08:34:01| cri

Maonesho ya pili ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yafunguliwa_fororder_aa

Maonesho ya pili ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yamefunguliwa jana huko Changsha, mkoani Hunan nchini China, na nchi zaidi ya 40 na makampuni karibu 900 za China na Afrika zimeshiriki kwenye maonesho hayo.

Kwenye ufunguzi wa maonesho hayo, Umoja wa Majukumu ya Kijamii kwa Makampuni ya China barani Afrika umeanzishwa, ambao umeshirikisha zaidi ya makampuni 1,700 ya China barani Afrika.

Licha ya baraza la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, mikutano na shughuli mbalimbali zitafanyika kwenye maonesho hayo. Washiriki watajadiliana kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye vyakula na mazao ya kilimo, maendeleo ya afya, ushirikiano wa miundombinu na ushirikiano wa mnyonyoro wa uzalishaji wa viwanda.