Waraka waonyesha kuwa nguvu ya uchumi wa China imeongezeka kwa kiwango kikubwa
2021-09-28 10:59:42| cri

Waraka uliotolewa na ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China yenye kichwa “Safari ya China kutoka umaskini hadi kwenye neema” unasema nguvu ya uchumi wa China imeongezeka kwa kiwango kikubwa, huku pato lake la taifa likiwa limeongezeka kutoka Yuan bilioni 67.9 kwa mwaka 1952, na kufikia Yuan trilioni 101.6 (Dola za kimarekani trilioni 15.5), katika kipindi hicho pia pato la mtu mmoja moja limeongezeka kutoka dola 100 za kimarekani kwa mwaka hadi dola elfu 10 za kimarekani.

Mbali na maendeleo ya kiuchumi, China pia imepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya kijamii, ikiwa imepata maendeleo makubwa kwenye huduma za chakula, afya, elimu, utalii, utamaduni na burudani, na sasa wachina wanatumia nusu ya mapato yao kwenye mambo hayo. Maendeleo hayo yametajwa kuwa ni hatua muhimu katika kuhusisha nguvu ya taifa na kufikia maendeleo ya kati kwa pande zote.  

Soko la ajira pia limeendelea kuwa tulivu na idadi ya ajira bora imekuwa ikiongeza. Idadi ya watu walioajiriwa imeongezeka kutoka watu milioni 180 wa mwaka 1949, hadi kufikia watu milioni 750 kwa mwaka 2020. Idadi ya wafanyakazi wenye ujuzi imefikia milioni 200, na kuonyesha ubora wa nguvu kazi ya China.