Bidhaa bora za Afrika zaingia kwenye familia za kawaida za China kupitia biashara ya kielektroniki
2021-09-28 08:58:41| cri

Bidhaa bora za Afrika zaingia kwenye familia za kawaida za China kupitia biashara ya kielektroniki_fororder___172.100.100.3_temp_9500049_1_9500049_1_1_93bd7ff0-597c-4eec-96c1-b1090e0054d7

Maonyeshao ya kwanza ya matangazo ya moja kwa moja ya biashara ya kielektroniki kati ya China na Afrika imefanyika juzi huko Changsha.

Kupitia maonyesho hayo, bidhaa bora mbalimbali kutoka Afrika zimeingia kwenye familia za kawaida nchini China kupitia matangazo ya watu mashuhuri kwenye mtandao wa Internet. Bidhaa hizo ni pamoja na kahawa kutoka Ethiopia, ufuta kutoka Tanzania, pilipili nyeupe kutoka Cameroon, na divai nyekundu kutoka Afrika Kusini.

Hayo nimatangazo ya moja kwa moja ya kwanza kuhusu bidhaa za Afrika kwa pande zote katika historia, yaliunganisha raslimali za biashara, majukwaa ya biashara ya kielektroniki na njia za uuzaji. Pia maonyesho hayo yametoa mchango kwa kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya pande hizo mbili.