Viwanda elfu 17 kutoka ndani na nje ya China vitashiriki kwenye Maonesho ya 17 ya Kimataifa ya viwanda vya katuni ya China yatakayofanyika kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 4 mjini Hangzhou, nchini China.
Maonesho hayo yatakayovutia watu wengi, yatafanyika kwa kutumia sayansi na teknolojia mpya zikiwemo teknolojia ya 5G na data kubwa.