Zaidi ya nchi 60 zapinga kuingiliwa kwa maswala ya ndani ya China kwa kisingizio cha haki za binadamu
2021-09-28 08:44:48| cri

Zaidi ya nchi 60 zimetoa taarifa ya pamoja katika kikao cha 48 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, zikieleza kuunga mkono msimamo wa China juu ya maswala yanayohusiana na mambo ya Xinjiang, Hong Kong, na Tibet.

Kaika taarifa yao ziliyotoa ijumaa iliyopita, nchi hizo pia zimeeleza kupinga kitendo cha baadhi ya nchi kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, baadhi ya nchi za magharibi zinatua kauli za kupotosha na kuingilia mambo ya ndani ya China, jambo linalopingwa na nchi nyingi zinazoendelea.