China yapinga kutafuta faida na kutumia vigezo viwili juu ya Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia
2021-09-28 14:21:57| cri

Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun jana alisema China inapinga kitendo cha kutafuta faida na kutumia vigezo viwili juu ya Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia (NPT).

Amesema Mkataba wa kupiga marufuku kwa pande zote majaribio ya nyuklia (CTBT) na Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia (NPT) yote miwili ni nguzo muhimu katika kuondoa silaha za nyuklia pamoja na mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia duniani. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhimiza mkataba wa CTBT uanze kutekelezwa haraka iwezekanavyo, pia inapaswa kulinda mamlaka, mambo ya ulimwengu na ufanisi wa mkataba wa NPT.

Ameongeza kuwa nchi zote zinatakiwa kuwa na msimamo wa kuwajibika.