Chanzo cha virusi vya Corona chapaswa kuchunguzwa dunia nzima ili kujilinda na janga
2021-09-28 15:37:08| Cri

Jarida la THE LANCET limesema chanzo cha janga la virusi vya Corona kimekuwa kikifuatiliwa duniani tangu lianze kuripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye jamii ya kimataifa mapema Januari, 2020. Tafiti nyingi zilizofanywa na wanasayansi duniani zinaonesha kuwa hakuna uwezekano wa virusi hivi kwamba vinatoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na havina uwezekano kabisa wa kuvuja kwenye maabara.

Hata hivyo jarida hilo limesema utafiti na taasisi za afya duniani bado hazijapata ufumbuzi wa wazi kuhusu maambukizi ya virusi hivi yalifika kwa binadamu kwa njia ipi, muda gani na mahali gani. Aidha limesisitiza kuwa hakuna ushahidi wala takwimu zinazounga mkono dhana ya kwamba virusi vya Corona ni vya kutengeneza.