Waziri wa mambo ya nje wa China atoa hotuba kwenye mkutano kuhusu “Kazi ya China katika Umoja wa Mataifa”
2021-09-28 14:22:31| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alitoa hotuba kwa njia ya video kwenye mkutano unaohusu “Kazi ya China katika Umoja wa Mataifa”.

Wang amesema mwaka huu inatimia miaka 50 tangu Jamhuri ya Watu wa China irejeshewe kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa. Katika miaka hiyo 50, China imetekeleza kihalisi malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kushikilia kulinda mamlaka halali ya nchi zinazoendelea, na imekuwa nchi muhimu katika kujenga amani ya dunia, kutoa mchango kwa maendeleo ya dunia, kulinda kithabiti utaratibu wa kimataifa, na kujitahidi kutoa bidhaa za umma.

Amesisitiza kuwa rais Xi Jinping wa China ametoa pendekezo juu ya maendeleo ya dunia katika mjadala wa kawaida wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambaye ametoa mwelekeo wa maendeleo kwa nchi mbalimbali. China itashirikiana na nchi mbalimbali duniani kuhimiza kihalisi ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Siku hiyo Bw. Wang Yi alipozungumza na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres kwa njia ya video alisema, China siku zote inazingatia ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na itaendelea kulinda kithabiti kanuni za Katiba ya Umoja huo, na mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuonesha umuhimu wake katika mambo ya kimataifa.