Mazungumzo ya 11 ya kimkakati kati ya China na Umoja wa Ulaya yafanyika
2021-09-29 09:03:28| Cri

Mazungumzo ya 11 ya kimkakati ya ngazi ya juu kati ya China na Umoja wa Ulaya yafanyika_fororder_src=http___i.guancha.cn_news_mainland_2021_09_29_20210929070154413.jpg&refer=http___i.guancha

Waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi na mwakilishi wa juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za diplomasia na usalama Jose Borrell jana wameendesha mazungumzo ya 11 ya kimkakati ya ngazi ya juu kati ya China na Umoja wa Ulaya kwa njia ya mtandao, na kuhimiza pande hizo mbili kuchangia juhudi za kimataifa katika kukabiliana na changamoto ya pamoja.

Wang Yi amesema, hivi karibuni mawasiliano na mazungumzo kati ya pande hizo mbili yameongezeka, hali itakayosaidia kukuza maelewano na kudhibiti mvutano. Ameongeza kuwa China inapenda kuendelea kukuza mawasiliano na Umoja wa Ulaya, na kuchukulia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama nguzo ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Kwa upande wake, Borrell amesema Umoja wa Ulaya unaichukulia China kama ni mwezi muhimu wa kimkakati, na unapenda kushirikiana na China kuandaa mawasiliano ya viongozi ya siku zijazo, na kutoa mwongozo wa kisiasa kwa maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.