Mkuu wa WHO aomba radhi kwa ukatili wa kingono uliofanywa na wafanyakazi wake nchini DR Congo
2021-09-29 10:44:13| cri

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus jana Jumanne aliomba radhi baada ya wachunguzi wa kujitegemea kuchunguza madai ya ukatili wa kingono nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) uliofanywa na wafanyakazi wa shirika hilo, akilaani vitendo hivyo na kusema huko ni "kushindwa kimuundo" na ni "uzembe wa mtu binafsi".

Amesisitiza kuwa kipaumbele chake ni kuhakikisha wahusika wote wanawajibishwa kisheria. Vitendo hivyo vilifanywa na wafanyakazi walioajiriwa nchini humo pamoja na wajumbe wa timu za kimataifa ambao walikuwepo nchini humo kupambana na mlipuko wa Ebola kutoka mwaka 2018 hadi 2020.