Jamaa mmoja nchini India anayeshutumiwa kutaka kubaka apewa dhamana kwa sharti la kufua nguo za wanawake kwa miezi sita
2021-09-29 10:44:45| cri

Jamaa mmoja nchini India ambaye anashutumiwa kwa kutaka kubaka amepewa dhamana kwa sharti la kufua na kupiga pasi nguo za wanawake wote kijijini kwake kwa miezi sita

Lalan Kumar, 20, atalazimika kununua sabuni na vifaa vingine vinavyohitajika ili kuwapatia huduma ya bure wanawake hao wapatao 2,000 ya kufuliwa nguo zao kwa miezi sita katika kijiji cha Majhor jimbo la Bihar. Kumar, ambaye kazi yake pia ni dobi, alikamatwa Aprili akishtakiwa kwa kutaka kumbaka, Santosh Kumar Singh ambaye ni afisa wa polisi wa Bihar wilaya ya Madhubani. Wanawake wote kijijini wamefurahia uamuzi wa mahakama. Tarehe ya kusikilizwa kesi bado haijapangwa.