UNDP yaitaka Afrika kufuata teknolojia za kidijitali ili kuongeza kasi ya kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu
2021-09-29 09:07:30| cri

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limezitaka nchi za Afrika kufuata teknolojia za kidijitali ili kuongeza kasi ya kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa itakapofika mwaka 2030.

Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Kenya Walid Badawi, ameliambia jukwaa la Afrika jijini Nairobi kuwa, teknolojia za kidijitali zitasaidia kuongeza kasi ya maendeleo kwa kuwa zinawezesha uratibu kwa wadau wengi katika njia tofauti ambazo awali hazikuwezekana.

Amesema moja ya njia za kutimiza Malengo hayo ya Umoja wa Mataifa ni kutambua na kutoa kipaumbele kwa malengo ya maendeleo endelevu ambayo yatakuwa na athari kubwa katika kutimiza malengo mengine.