Rais wa China aagiza kuharakisha ujenzi wa kituo cha watu muhimu wenye ujuzi
2021-09-29 08:59:24| cri

 

 

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, inapaswa kutekeleza mkakati wa kuifanya China kuwa na nguvu kwa kupitia watu wenye ujuzi, na kuharakisha ujenzi wa kituo cha watu muhimu wenye ujuzi na mazingira ya uvumuzi.

Akizungumza katika mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi za watu wenye ujuzi, Rais Xi amesema, China inakaribia kufikia lengo kuu la kutimiza ustawi mkubwa wa taifa kuliko kipindi chochote katika historia, pia inahitaji zaidi watu wenye ujuzi kuliko kipindi chochote. Ili kutimiza lengo hilo, China lazima ijiendeleze pamoja na sayansi na teknolojia za kiwango cha juu, na ni lazima itambue changamoto zake, itilie maanani zaidi kutoa mafunzo kwa watu wenye kipaji, na kuharakisha kuanzisha mazingira mazuri ya kuvutia rasilimali ya watu wenye ujuzi.