EABC yasema ufufukaji baada ya janga la COVID-19 uko katika mwelekeo mzuri
2021-09-30 08:53:05| CRI

 

 

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limesema, ufufukaji wa uchumi kutokana na athari zinazohusiana na janga la virusi vya Corona katika kanda hiyo unaendelea vizuri, wakati vizuizi vya usafiri vikilegezwa, utoaji wa chanjo kuongezka, na kurejesha imani kwa wawekezaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa EABC John Bosco Kalisa amesema, serikali katika kanda hiyo zimefanya maamuzi ya sera za kijasiri ili kuharakisha ufufukaji wa sekta muhimu kama utalii, kilimo na uzalishaji, ambazo ziliporomoka wakati wa kilele cha janga hilo.

Katika jukwaa lililoitishwa na Baraza hilo kujadili ufufukaji wa biashara na uwekezaji katika kanda hiyo, Kalisa amesema kwa sasa wanashughulikia mkakati wa ufufukaji baada ya COVID-19, wakilenga sekta zenye athari kubwa kiuchumi na kwa maisha ya watu wa kanda hiyo.