Algeria yaanza kutengezena chanjo za Corona za Sinovac
2021-09-30 10:42:40| cri

Algeria jana ilianza kutengeneza chanjo za Corona za Sinovac ikiingia ubia na kampuni ya China iliyoko mkoani Constantine, mashariki mwa Algeria.

Shughuli hiyo imeanzishwa katika hafla iliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya utengenezaji wa dawa ya kibiolojia ya China Sinovac Biotech na Kampuni ya utengenezaji wa dawa ya Algeria Saidal. Waziri mkuu wa Algeria Bw. Ayman Benabderrahmane na balozi wa China nchini Algeria Bw. Li Lianhe wameshiriki kwenye hafla hiyo.

Benabderrahmane ametoa hotuba akisema mradi huo unatarajiwa kutandika njia ya kutengeneza chanjo nyingine katika siku chache za baadaye, pia utaifanya Algeria izidi kujitosheleza kwa chanjo za Corona pamoja na usalama wa afya .

Kwa upande wa China, balozi Li amesema kukamilika kwa mradi huo ni hatua muhimu kwenye historia ya ushirikiano kati ya China na Algeria, ambazo zina urafiki mkubwa na msimamo mmoja juu ya masuala mengi.