Shirikisho la China latoa mabegi ya shule kwa wanafunzi wahitaji nchini Ethiopia
2021-09-30 08:52:26| CRI

Shirikisho la China latoa mabegi ya shule kwa wanafunzi wahitaji nchini Ethiopia_fororder_3eeb410674e94de8b34017e9c5afdb4e

Mfuko wa Kuondoa Umasikini wa China (CFPA) umetoa mabegi 20,000 ya shule kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji nchini Ethiopia, na pia kuzindua Mradi wa Mfuko wa Panda (2021-2022) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu nchini Ethiopia.

Msaada huo wa mabegi ya shule ni mwendelezo wa ubunifu wa CFPA, ambao umewanufaisha karibu 98,000 wa Ethiopia kuanzia mwaka 2019.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, Waziri wa Elimu wa Ethiopia Getahum Mekuria ameishukuru China kwa kuendelea kuiunga mkono Ethiopia, kutoka sekta ya elimu hadi ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, na pia mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

Kwa upande wake, katibu wa kwanza wa Ofisi ya masuala ya Uchumi na Biashara katika Ubalozi wa China nchini Ethiopia, Liu Keyi amesisitiza tena kuwa Ubalozi huo utaendelea kuboresha ushirikiano wa kina wa pande mbili katika sekta ya elimu na sekta nyingine.