Fumio Kishida kuwa waziri mkuu mpya wa Japan
2021-09-30 09:02:02| cri

Uchaguzi wa rais wa Chama cha Kidemokrasia cha Japan ulifanyika jana mjini Tokyo, ambapo waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Fumio Kishida, alishinda uchaguzi huo na kuwa rais wa 27 wa Chama hicho.

Kwa mujibu wa Katiba ya Japan, akiwa mkuu wa chama tawala, Bw. Fumio atachukua nafasi ya Bw. Yoshihide Suga kuwa waziri Mkuu mpya wa Japan katika mkutano wa bunge la mpito utakaofanyika tarehe 4, mwezi ujao.