Rais wa China atoa heshima kwa mashujaa wa taifa katika Uwanja wa Tian'anmen
2021-09-30 10:30:57| cri

Rais wa China atoa heshima kwa mashujaa wa taifa katika Uwanja wa Tian'anmen_fororder_现场图3

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine wa ngazi ya juu wametoa heshima na kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa la China katika Uwanja wa Tian'anmen hapa Beijing.

Mwezi Agosti mwaka 2014, Bunge la Umma la China lilipitisha uamuzi wa kuweka tarehe 30, Septemba kuwa Siku ya Kuwakumbuka Majushaa. Kuanzia hapo, siku hiyo kila mwaka, China inafanya shughuli ya kuwakumbuka na kutoa heshima kwao kwa jina la taifa ili moyo wa kishujaa uhifadhiwe katika kumbukumbu ya taifa.