FAO yatoa wito wa kupunguza upotezaji wa chakula
2021-09-30 10:43:28| cri

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Bw. Qu Dongyu ametoa wito kwa nchi zote kuongeza juhudi za kupunguza kutupa chakula kwa nusu hadi mwishoni mwa muongo huu.

Shirika hilo lilikadiria kuwa karibu asilimia 14 ya a chakula chote duniani kimepotea kwenye mavuno na rejareja, kikigharimu dola za kimarekani bilioni 400 kwa thamani ya chakula kila mwaka.

Bw. Qu ameongeza kuwa mifumo bora zaidi, ambayo ni jumuishi na endelevu ya kilimo na chakula itasaidia kupunguza njaa duniani na kupunguza shida kwa mazingira.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bw. Inger Andersen amesema kuwa upotezaji wa chakula na taka unachukua karibu moja ya kumi ya utoaji wa gesi chafu duniani, wakati wa kutumia rasilimali za ardhi na maji.