Thamani ya miradi iliyosainiwa kwenye CAETE yafikia dola bilioni 22.9 za Kimarekani
2021-09-30 08:49:16| CRI

Thamani ya miradi iliyosainiwa kwenye CAETE yafikia dola bilioni 22.9 za Kimarekani_fororder_VCG111351348211

Maonesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika (CAETE) yamefungwa jana mjini Changsha, China, na takwimu zinaonesha kuwa, thamani ya miradi 135 ya ushirikiano iliyosainiwa kwenye maonesho hayo ilifikia dola bilioni 22.9 za Kimarekani.

Naibu katibu mkuu wa sekretariati ya kamati ya maandalizi ya maonesho hayo Shen Yumou, amesema, kutokana na juhudi za pande mbalimbali, maonesho hayo yamepata mafanikio makubwa, hatua kadhaa mpya za ushirikiano kati ya China na Afrika zimetekelezwa, na idadi na thamani ya miradi iliyosainiwa vimeongezeka kuliko maonesho ya kwanza.

Maonesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika ni sehemu muhimu ya “Hatua Nane” za ushirikiano kati ya pande hizo mbili zilizotangazwa kwenye Mkutano wa FOCAC uliofanyika mjini Beijing mwaka 2018.

Maonesho hayo yanafanyika kila baada ya miaka miwili, na yamekuwa jukwaa muhimu la ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika katika mambo ya uchumi na biashara.